Kundi la wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan limemteua kiongozi mpya baada ya kuuawa kwa Mullah Mansour.
Bw Mawlawi Haibatullah Akhundzada ndiye kiongozi mpya.
Manaibu wake watakuwa Sirajuddin Haqqani, ambaye mtandao wake umedaiwa kutekeleza mashambulio mengi ya mabomu Kabul, na Mohammad Yaqoob, mwanawe mwanzilishi wa Taliban, Mullah Omar.
Mansour aliuawa katika mkoa wa Balochistan nchini Pakistan kwenye shambulio lililotekelezwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani.
Rais wa Marekani Barack Obama Jumatatu alithibitisha kifo cha Mansour Jumatatu.
Pentagon ilisema Mansour amekuwa akipanga mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Jumanne, waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan aliambia wanahabari kwamba mwili wa Mansour ulipatikana karibu na mpaka wan chi hiyo na Pakistan.
Post a Comment