0





Na.Alex Mathias
Baada ya kuifunga Yanga magoli mawili peke yake Mshambuliaji wa JKU, Emmanuel Martin wa JKU amesaini mkataba wa miaka miwli kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani.
Mshambuliaji huyu anatarajia kuanza mazoezi na wenzake siku ya kesho kujiandaa na Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzani bara unaotarajiwa kuanza siku ya Jumamosi ya Desemba 17,2016 huku Mabingwa hao wanatashuka dimba kucheza Jkt Ruvu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kusajiliwa kwa Mshambuliaji huyu kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa huku mchezaji wa kwanza akiwa ni kiungo mkabaji Justine Zulu ambaye ametokea klabu ya Zesco United ya Zambia huku ikiwa imemuacha mchezaji mmoja aliyemaliza mkataba wake Mbuyu Twitte.
Kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Deusdedit amesema kuwa katika dirisha dogo wameweze kusajili wachezaji wawili tu yakiwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi ambalo linaongozwa na kocha mkuu George Lwandamina akishirikiana na Mkurugenzi wa Ufundi Hans Van Der Pluijm.


Kwa upande wa wekundu wa Msimbazi wametoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kama unavyoona hapo chini.

Klabu ya Simba inapenda kutangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog.
Kwenye maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu
Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, pamoja na Emmanue Semwanza atakaekwenda Majimaji ya Songea,
Huku pia klabu ikiachana rasmi na Golikipa muaivory coast Vicent Agban na kiungo Mcongo,Mussa Ndusha.
Sambamba na kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James kotei, huku tukikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Luizio anayekuja kwa mkopo toka Zesco ya Zambia.
Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Ali kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta kwetu kwa mkopo.
Tunaamini maboresho haya yataongeza chachu ya ushindani ktk kikosi chetu na Hatimaye kutupa mataji msimu huu.
Niwaarifu pia timu yetu imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda FC, mchezo utakaopigwa siku ya Jumapili ya tarehe 18/12/2016 huko Mtwara.
Imetolewa na ;
Haji S. Manara
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA

Post a Comment

 
Top